Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hadhi ya kuwa Mkimbizi kwa Wakimbizi nchini Angola na Liberia kufikia kikomo mwezi huu

Hadhi ya kuwa Mkimbizi kwa Wakimbizi nchini Angola na Liberia kufikia kikomo mwezi huu

Wakimbizi wanaoishi kwenye mataifa ya Angola na Liberia huenda wakapoteza hadhi za kuwa wakimbizi itimiapo tarehe 30 mwezi huu. Kunzia wakati huo wakimbizi wanaoishi kwenye nchi hizo mbili hawatambuliwa kama wakimbzi na shirika la kuwahudumia wakimbzi la Umoja wa mataifa UNHCR na pia serikali zinazowapa hifadhi.

Nchini Liberia wakimbizi waliolikimbia taifa hilo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye kati ya mwaka 1989 na mwaka 2003 watapoteza hadhi ya kuwa wakimbizi. Vita nchini Liberia vilisabaisha vifo vya watu 250,000 na wengine 750,000 kuhama makwao. Nchini Angola wakimbizi ambao watapoteza hadhi ni wale walioihama nchi hiyo kati ya mwaka 1965 na 1975 wakati wa vita vya kupigania uhuru kutoka koloni la Ureno na vita vya wenywe kwa wenye hadi mwaka 2002. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(CLIP  YA ADRIAN EDWARDS )