Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya Marekani kuhusu Afya inaweza Kupunguza Mwanya katika Usalama wa Kijamii:ILO

Sheria ya Marekani kuhusu Afya inaweza Kupunguza Mwanya katika Usalama wa Kijamii:ILO

Shirika la Ajira Duniani, ILO, limesema sheria ya kubadili mfumo wa huduma za afya Marekani inaweza kusaidia kupunguza mwanya wa usalama wa kijamii, ambao kwa sasa unawaathiri hadi watu milioni 30 kote nchini.

Mratibu wa sera za afya katika idara ya usalama wa kijamii ya ILO, Dr. Xenia Scheil-Adlung, amesema sheria hiyo mpya bila shaka itawasaidia watu ambao kwa sasa hawana namna ya kupata huduma za afya, na hivyo, inakwenda sambamba ba juhudi za ILO za kupanua usalama wa kijamii kote duniani.

Mtaalam huyo wa ILO amesema, mjadala ambao umeibuka Marekani kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu zaidi kuihifadhi sheria hiyo, ni mzuri. Alice Kariuki na taarifa kamili