Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yahofia Usalama wa Chakula Kenya kufuatia Uhaba wa Mvua

WFP yahofia Usalama wa Chakula Kenya kufuatia Uhaba wa Mvua

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema hali ya usalama wa chakula nchini Kenya inatia wasiwasi kufuatia ukame uliofuatiwa na kiwango cha chini cha mvua. Kutokana na hali hiyo, ukaguzi uliofanywa mwezi Juni unaonyesha kuwa hadi watu milioni 2.4 watakumbwa na uhaba wa chakula, kufuatia mvua haba kati ya mwezi Machi na Mei. Maeneo ya kusini mashariki na pwani ya Kenya ambayo hayafanyi ukulima kwa kiasi kikubwa na ambayo hutegema misimu mifupi ya mvua kwa ukulima, pia yalikuwa na ukame kati ya mwezi Oktoba na Disemba. Shirika hilo limesema litafanya ukaguzi wa kina kuhusu usalama wa chakula mwezi Agosti.

Shirika la WFP pia limekuwa likiendelea kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi 560, 000 katika kambi za Dadaab na Kakuma, ambazo zinaendelea kupokea wakimbizi kila uchao. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(CLIP YA ELISABETH BYRS)