Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP Kuongeza Msaada wa chakula Sudan Kusini

WFP Kuongeza Msaada wa chakula Sudan Kusini

Baada ya kuwasaidia zaidi ya watu 1.9 Sudan Kusini, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, linapanua utoaji wa msaada kwa watu zaidi wanaokabiliwa zaidi na tishio la njaa, wakati msimu wa njaa ukiendelea. Shirika hilo limepanga kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni 2.9 mwaka huu, kupitia ugawaji wa kawaida, na shughuli za kuchagiza lishe bora, chakula kwa watoto wa shule na miradi ya kutoa chakula kwa taasisi.

Likishirikiana na wadau wengine, shirika la WFP hutoa biskuti za kuongeza nguvu na kiasi cha muda cha chakula kwa watu wanaowasili upya, hadi hapo wanapoandikishwa kama wakimbizi na kuanza kupokea chakula cha mwezi mzima, kulingana na idadi ya watu katika familia moja. Shirika hilo litalenga watoto 600, 000, wanawake waja wazito na wanaonyonyesha watoto kwa kuwapa lishe wanayohitaji.