Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara lazima Ziheshimu Haki za Binadamu kwa Maendeleo Endelevu ya uhakika:Rio+20

Biashara lazima Ziheshimu Haki za Binadamu kwa Maendeleo Endelevu ya uhakika:Rio+20

Chombo cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa kinachohusika na kuchagiza biashara zote kuheshimu haki za biinadamu katika sekta zote na katika nchi zote kimeelezea hofu kuhusu hati ya matokeo ya mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20.

Chombo hicho kinasema hati hiyo imeshindwa kueleza kwamba biashara lazima ziheshimu haki za binadamu katika juhudi za kuelekea uchumi unaojali mazingira na maendeleo endelevu.

Kwa mujibu wa mkuu wa chombo hicho Puvan Selvanathan amesema biashara zitakuwa na jukumu kubwa katika kuleta maendeleo yanayojali mazingira na kulinda haki za binadamu ni muhimu sana ili kuhakikisha kwamba sera na mipango ya biashara ina malengo ya kulinda mazingira, kuleta maendeleo na sio kuathiri watu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)