Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban anatumai Mkutano wa Geneva utakuwa Mwanzo wa Mabadiliko kwa Mgogoro wa Syria

Ban anatumai Mkutano wa Geneva utakuwa Mwanzo wa Mabadiliko kwa Mgogoro wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasafiri kuelekea Geneva Ijumaa ya leo ili kuhudhuria mkutano Jumamosi wa kundi la kuchukua hatua dhidi ya hali inayoendelea Syria.

Mkutano huo umeitishwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu Syria Kofi Annan,na unafanyika wakati ambapo mgogoro wa Syria umeshika kasi na watu zaidi ya 10,000 wameshauawa tangu Machi 2011.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama ambao ni Uchina, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani wamealikwa. Mwaliko pia umetumwa kwa Katibu Mkuu wa Muungano wan chi za Kiarabu , Nabil Elaraby na mwakilishi wa mambo ya nje na sera za usalama wa Muungano wa Ulaya .Wengine walioalikwa ni mawaziri wa mambo ya nje wa Iraq, Kuwait, na Qatar.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Alhamisi Ban amesema anatumaini kundi la kuchukua hatua litakuwa chachu ya mabadiliko katika hatua za pamoja za kukabiliana na mgogoro wa Syria.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“Makundi haya ni wadau muhimu katika kutatua mzozo wa Syria. Hivyo ninatumai kwamba tutaweza kuleta msukumo, na kuchagiza maamuzi kwa misingi ya kuweza kusonga mbele na utekelezaji wa vipengee sita vya mpango wa amani”