Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP Yaanza kutoa Vocha za Chakula kwa Wakimbizi wa Syria, Lebanon

WFP Yaanza kutoa Vocha za Chakula kwa Wakimbizi wa Syria, Lebanon

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, limeanza kutoa vocha za chakula ili kuwasaidia wakimbizi 40, 000 wa Syria, walioko kwenye bonde la Bekaa nchini Lebanon, kama sehemu ya operesheni ya kikanda ya dharura ya kuwasaidia raia wa Syria walokimbia machafuko nchini mwao.

Kupitia mpango huu wa kutoa vocha, WFP inakadiria kuwafikia wakimbizi 27, 000 walioko Lebanon ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai, ikiwa na mpango wa kuwafikia hadi wakimbizi 40, 000 kabla ya mwisho wa mwaka. Mpango wa kutoa vocha kwa wakimbizi unwasaidia i kununua chakula kutoka kwa maduka ya wenyeji, na hivyo kuchangia uchumi ya wenyeji.

Shirika la WFP liaongeza juhudi zake za kutoa msaada kwa wakimbizi 120, 000 katika nchi jirani za Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki. Tayari mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine, yametoa ombi la dola milioni ili kuwasaidia wakimbizi wa Syria ambao wanaongezeka.