Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICTY yatupilia mbali maombi 10 ya Karadzic ya kuondolewa mashtaka yote 11

ICTY yatupilia mbali maombi 10 ya Karadzic ya kuondolewa mashtaka yote 11

Mahakama nambari tatu kuhusu uhalifu wa kivita katika taifa la zamani la Yugoslavia (ICTY), imefutilia mbali maombi kumi kati ya kumi na moja ya Radovan Karadžić kutaka asishtakiwe. Hata hivyo, mahakama hiyo imekubali ombi lake kuondolewa shtaka kuhusu mauaji ya kimbari, kutokana na makosa anayoshukiwa kufanya kati ya mwezi Machi na Disemba mwaka 1992 katika miji mingi ya Bosnia na Herzegovina.

Kuondolewa shtaka hilo kunafuatia kutokuwepo ushahidi wa kutosha kumshtaki Bwana Karadzic kwa mauaji ya kimbari, kulingana na sheria nambari 98 ya uendeshaji mashtaka mahakama hiyo.

Karadzic, ambaye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la Kiserbia Bosnia, amekuwa akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari, uahalifu dhidi ya binadam, na ukiukaji wa sheria za kivita, makosa ambayo yalitendeka Bosnia na Herzegovina kati ya 1992 na 1995.