Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna Taifa pekee linaloweza kuushinda Ugaidi:Nassir

Hakuna Taifa pekee linaloweza kuushinda Ugaidi:Nassir

 

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulaziz Al-Nasser amesema hakuna taifa hata moja hata liwe na nguvu kiasi gani linaloweza kupambana na ugaidi peke yake. 

Akizungumza katika siku ya pili ya kongamano la kupambana na ugaidi kwenye Baraza Kuu Bwana Al-Nasser amesema jumuiya ya kimataifa imepiga hatua kubwa na kupata mafanikio katika vita dhidi ya ugaidi hali inayodhihirisha kwamba dunia ina ari na moyo wa kushirikiana hata wakati ambao inakabiliwa na changamoto kubwa. 

Ameongeza kuwa nguzo nne muhimu zinashughulikia masuala muhimu ya kupambana na ugaidi kimataifa. Ameongeza kuwa wakati umewadia wa kuwa na utekelezaji madhubuti wa miakakati iliyoweka ya vita dhidi ya ugaidi. 

(SAUTI YA AL-NASSER)