MONUSCO yaongezewa Muda nchini DRC

28 Juni 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha muda wa kusalia nchini Congo vikiso vya kimataifa MUNUSCO vinavyoendesha operesheni ya amani. Vikosi hivyo sasa vimeongezewa muda wa mwaka mmoja mwingine utakaotumika kuboresha mazingira ya hali ya usalama.

Pamoja na kuongeza kwa kipindi hicho, baraza hilo la usalama limeitolea mwito serikali ya Congo kufanyia mageuzi sekta yake ya usalama ili kuzikabili changamoto ndogo ndogo zinazoendelea kuibuka.

Vikosi hivyo vya usalama vitasalia nchini Congo hadi June 30,2013 na vitakuwa na shabaha ya kuimarisha hali ya usalama.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter