Mkutano wa Rio watambua Umuhimu wa Mkataba wa CITES

28 Juni 2012

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu wa Rio+20 umeitambua makala moja inayozungumzia umuhimu wa mkataba kuhusu biashara ya kimataifa kwa viumbe vilivyo kwenye hatari ya kuangamia.

Makala hiyo ilipitishwa na wanachama wa Umoja wa Mataifa tarehe 22 mwezi huu na imetajwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kama inayotoa mwelekeo mpya. Kwa sasa kuna watu bilioni sana duniani wanaotumia bayo anuai kila siku kupitia njia za madawa, chakula , nguo , marashi na vitu vingine vya kifahari.

Mkurugenzi mkuu wa mkataba huo ujulikanao kama CITES John E Scalnon amesema kuwa mkataba huo ulioanza kutekelezwa mwaka 1973 unahitajika sasa kuhakikisha kuwa biashara ya viumbe vilivyooordheshwa kuwa hatarini imeharamishwa.