Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Washirika wake Wanaomba Dola Milioni 193 Kusaidia Wakimbizi wa Syria:UNHCR

UM na Washirika wake Wanaomba Dola Milioni 193 Kusaidia Wakimbizi wa Syria:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na washirika wengine wadau wametoa ombi Alhamisi la fedha za haraka ili kusaidia kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya wakimbizi wa Syria inayoongezeka Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq.

Mashirika hayo mwezi Machi yaliomba dola milioni 84.1 lakini ynasema ongezeko la wakimbizi linamaanisha wanahitaji fedha zaidi na dola milioni 193 ndio zitakazosaidia kwa sasa. Kwa mujibu wa mratibu wa UNHCR kanda ya Mashariki ya Kati nchi zinazohifadhi wakimbizi hao yaani Lebanon, Jordan, Uturuki na Iraq zimejitolea na kuonyesha moyo wa ukaribu hivyo jumuiya ya kimataifa lazima na muhimu kusaidia operesheni hizo za wakimbizi. Katika miezi mitatu iliyopita mashirika ya misaada yamekuwa yakiorodhesha wakimbizi wa Syria wastani wa 500 kwa siku na wakimbizi 96,000 ama wameandikishwa au wanahifadhiwa nchi jirani. UNHCR inasema 50,000 kati yao sasa wanapokea msaada.

(SAUTI YA ……..)