Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao kuhusu Maadili kwenye Maendeleo Kuandaliwa

Kikao kuhusu Maadili kwenye Maendeleo Kuandaliwa

Juma moja baada ya kukamilika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu sasa kikao cha tume ya maadili, Sayansi na Teknolojia ulimwenguni kitatoa fursa kwa wataalamu, serikali na jamii ya wanasayansi kuweza kujadili ni kwa njia ipi madili yaweza kuchangia maendeleo endelevu kupitia sayansi na Teknolojia. Suala la mchango uliotolewa na sayansi na Teknolojia kwenye maendeleo ni suala lililotajwa mwisho wa mkutano wa Rio+20 lakini pia na changamoto zake kwa jamii. Tume hiyo itayazungumzia mambo manne muhimu kuhusu uhusiano uliopo kati ya Sayansi , Teknolojia na maendeleo endelevu yakimwemo maadili ya mabadiliko ya hali ya hewa, ya sayansi, kuhusu maendeleo na maadili yasiyo ya kiteknolojia.