Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wapoteza makazi kutokana na machafuko ya jimbo la Rakkhine, Myanmar

Wengi wapoteza makazi kutokana na machafuko ya jimbo la Rakkhine, Myanmar

Kiasi cha watu 52,000 wamekosa makazi kutokana na machafuko yaliyoibuka hivi karibuni katika jimbo la Rakkhine, nchini Myanmar ambayo yalisababisha mamia ya watu kuyahama makazi yao.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali watu hao sasa wamepatiwa hifadhi katika vijiji vipatavyo 66. Wakati wa machafuko hayo yaliyoanza May 28 watu 50 walipoteza maisha huku wengine 54 wakijeruhiwa na kunaripoti pia za kuvunjwa kwa jumba zipatazo 2230.

Serikali imetangaza hali ya hatari katika maeneo kadhaa ikiwemo huku ikiimarisha hali ya ulinzi kwenye miji ambayo ilihusika pakubwa na machafuko hayo.

Serikali imeomba mashirika ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuwakirimu waathirika wa matukio hayo.