UNDP Yazindua Machapisho yanayomulika Maendeleo ya Dunia

27 Juni 2012

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limezindua chapisho lake la rangi lilaolezea mafanikio iliyoyapata wakati ikitekeleza majukumu yake ya kimaendeleo duniani kote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa machapisho hayo 18, mtendaji mkuu wa shirika hilo Bi Helen Clark amesema kuwa,jambo la kutiliwa maanani kwenye machapisho hayo ni namna yalivyoweza kugusa moja kwa moja maisha ya watu ambao ndiyo zingatio kubwa la ukifiaji wa shabaha ya kimaendeleo.

Machapisho hayo yametuwama kwenye maeneo mbalimbali kuanzia yale yanayohusu mazingira, maendeleo kwa umumla, masuala ya siasa na haki za msingi mpaka kwenye shughuli za kilimo na uwajibikaji.

Pamoja na kutoa hali halisi ya maendeleo ya mataifa mbalimbali duniani, machapisho hayo lakini pia yanatoa sisitiza kwa nchi wahisani namna zinavyopaswa kujenga mashirikiano mema na taasisi za kidola wakati zinapokaribisha mashirikiano.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter