Idadi ya Wapalestina walioathirika na bomoabomoa ya Israel Inaongezeka:Falk

27 Juni 2012

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa Richard Falk ameonya Jumatano kwamba idadi ya watu walioathirika na bomoabomoa ya majengo ya Wapalestina imeongezeka kwa asilimia 87 ikilinganishwa na mwaka jana.

Bwana Falk pia ameitaka serikali ya Israel kusitisha mara moja ubomoaji wa nyumba za Wapalestina na kuanza kutimiza wajibu wake wa kulinda haki za kuwa na nyumba.

Ameongeza kuwa mwaka huu pekee tayari uongozi wa Israel uumeshabomoa zaidi ya majengo ya Wapalestina 330 zikiwemo nyumba, makazi ya mifugo, visima vya maji na barabara.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter