Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali na Majeshi ya Upinzani Wanakiuka Haki za Binadamu Syria

Serikali na Majeshi ya Upinzani Wanakiuka Haki za Binadamu Syria

Ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na majeshi ya serikali na makundi ya upinzani Syria unaongezeka wakati mapigano yakisambaa nchi nzima limeelezwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Jumatano.

Katika ripoti yake kwa baraza tume ya uchunguzi kuhusu Syria imesema jeshi la serikali na washirika wake wamehusika na mauaji ya raia , kuwatia kizuizini na mifumo mingine ya utesaji, huku makundi ya upinzani yamekuwa yakiwatesa au kuwauwa wanajeshi wa serikali na wanaoshukiwa kusaidia serikali.

Tume hiyo imesema haiwezi kufuta dhana kwamba majeshi yanayounga mkono serikali huenda yaalihusika na mauaji ya halaiki ya Al-Houla ambako watu zaidi ya 100 waliuawa. Hata hivyo tume pia imesema inawezekana kwamba wapiganaji wanaopinga serikali au makundi ya kigeni yasiyojulikana yanaemuunga mkono yalitekeleza mauaji hayo. Paulo Pinheiro ni mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi

(SAUTI YA PAULO PINHEIRO)