Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utesaji bado upo, miaka 25 tangu Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Utesaji:Ban

Utesaji bado upo, miaka 25 tangu Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Utesaji:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema utesaji wa watu bado upo, miaka 25 tangu mkataba wa kimataifa wa kupinga utesaji kutiwa saini. Bwana Ban ameyasema haya katika ujumbe wake kwenye siku ya kimataifa ya kuwasaidia waathirika wa mateso.

Amesema kila siku, wanaume, wanawake na hata watoto, huteswa au kudhulumiwa na lengo la kuwadhalilisha na kuwaondolea hadhi na thamani yao ya utu. Amesema kuna baadhi ya mataifa ambayo serikali zake hutumia utesaji kama mbinu ya kuwafanya watu wawe na uoga.

Katika ujumbe wake, Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu, Navi Pillay amesema, utesaji kwa hali yoyote ile ni kinyume na sheria, na hauwezi kukubalika kwa vyovyote vile. Amesema mara nyingi waathirika wa utesaji huwa watu wa kawaida, ambao tayari ni miongoni mwa watu wanyonge katika jamii, wakiwemo watoto.