Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Rio + 20 waadhimia kuanzisha kituo cha mafunzo kwa ajili ya maendeleo endelevu

Mkutano wa Rio + 20 waadhimia kuanzisha kituo cha mafunzo kwa ajili ya maendeleo endelevu

Kuanzishwa kwa kituo maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo yahusuyo maendeleo endelevu ni alamu ya pekee itayokumbusha dunia juu ya mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa Rio +20.

Kwa mujibu wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, mapendekezo yaliyofikiwa juu ya uanzishwaji wa kituo hicho yanatoa alaamu muhimu juu ya hatua zilizopigwa na mkutano huo wa kimataifa uliomalizika mwishoni mwa wiki huko Rio de Jeneiro.

Wajumbe kwenye mkutano huo kwa pamoja walifikia makubaliano ya kiuanzishwa kwa kituo hicho ambacho kitakuwa na kazi ya kutoa mafunzo kuhusiana na maendeleo endelevu.

Pamoja na mambo mengine ya kitaaluma, kituo hicho kinatazamia kutoa miongozo ya utafiti ili kufanikisha mijadala mbalimbali inayohusu maendeleo endelevu.