Waziri wa afya nchini Sierra Leon ateuliwa mjumbe masuala ya dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo

25 Juni 2012

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Zainab Hawa Bangura ambaye kwa sasa ni waziri wa afya nchini Sierra Leone na mjumbe wake mpya kwenye masuala ya dhulama na kimapenzi kwenye mizozo. Bangura tachuka mahala pa Margot Wallstrom mwanasiasa kutoka Sweden aliye na historia ya kutetea haki za wanawake.

Kupitia kwa msemaji wake Ban amemtaja Bi Banagura kuwa aliye na tajriba ya miaka mingi kuhusu masusla ya kidiplomasia , usimamizi na utatuzi wa mizozo barani Afrika.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter