Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea wasiwasi uliopo kufuatia Kudunguliwa kwa Ndege ya Uturuki nchini Syria

Ban aelezea wasiwasi uliopo kufuatia Kudunguliwa kwa Ndege ya Uturuki nchini Syria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasi wasi uliopo kufuatia kudunguliwa kwa ndege ya kijeshi ya Uturuki nchini Syria. Akizungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya kigeni nchini Uturuki Ahmet Davutoglu Ban aliipongeza Uturuki kwa moyo wa uvumilivu ambao imeonyesha na pia kuyashukuru mataifa hayo mawili kwa oparesheni ya pamoja ya kuitafuta ndege hiyo.

Ban amezitaka nchi hizo mbili kusuluhisha suala hilo kwa njia za kidiplomasia. Kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa kwa sasa fikra zake ziko kwa familia kwa marubaini wa ndege hiyo ambao kwa sasa hawajulikani waliko akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada unaohitajika. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari ndege hiyo la kijeshi ya Uturuki ilidunguliwa na kombora lililovyatuliwa kutoka ardhini kwenye pwani ya Syria siku ya Ijumaa.