Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na Wasichana wengi Wanauawa nyumbani:Manjoo

Wanawake na Wasichana wengi Wanauawa nyumbani:Manjoo

Dhuluma dhidi ya wanawake zimeongezeka na kufikia viwango vya kutisha, huku wanawake na wasichana wengi zaidi wakiendelea kuuawa nyumbani na wachumba wao au jamaa zao, kwa mujibu wa mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Rashida Manjoo.

Mtaalam huyo wa masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake, amesema katika mataifa mengi, nymbani ndipo mahali ambako uwezekano wa mwanamke kuuawa ni mkubwa zaidi, huku uwezekano kama huo wa kuuawa wanaume ukiwa kwenye barabara mitaani.

Katika ripoti yake, Bi Manjoo amesema, kuuawa kwa wanawake na wasichana ili kutakasa hadhi ya familia zao kunafanyika katika maeneo mengi duniani bila wahalifu kuchukuliwa hatua za kisheria. Amesema mataifa mengi yanashindwa kuwahakikishia wanawake haki ya kuishi bila dhuluma, na hivyo kuendeleza dhana kuwa dhuluma za wanaume dhidi ya wanawake ni inakubalika na ni lazima iwepo.

(SAUTI YA RASHIDA MANJOO)