Watu 7 wafariki katika ghasia zaidi Gaza na kusini mwa Israel - OCHA

22 Juni 2012

Shirika la kuratibu mipango ya dharura la Umoja wa Mataifa, OCHA, limesema kuwa kuongezeka kwa ghasia kwenye eneo la Gaza na kusini mwa Isarel kumepelekea kuuawa kwa WaPalestina 7, wakiwemo raia watatu, na kuwajeruhi Wapalestina wengine 14, na wanajeshi 4 wa Israel.

Zaidi ya watu 60, wakiwemo watoto 37, walilazimika kuhama kutoka jamii ya Bedouin, karibu na mji wa Bethlehem baada ya vikosi vya Israel kuvunja nyumba zao. Mgao wa umeme kwenye eneo zima la Gaza unaendelea kwa hata saa 12 kila siku, huku kuingia kwa mafuta kukiwa haba, na hivyo kufanya utoaji wa huduma muhimu kuwa mgumu, na hali ya maisha kuzorota.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter