Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM,USAID na PEPAFAR kupanua mradi wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa wahamiaji nchini Afrika Kusini.

IOM,USAID na PEPAFAR kupanua mradi wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa wahamiaji nchini Afrika Kusini.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM la USAID kupitia ufadhili wa mpango wa dharura wa rais wa Marekani PEPFAR wanatarajiwa kuongeza hadi mwaka 2016 mradi unaotoa huduma zinazohusiana na ugonjwa wa ukimwi kwa wafanyikazi wa shambani kwenye mikoa ya Limpopo na Mpumalanga nchini Afrika Kusini.

Mradi huo unaojulikana kam Ripfumelo II project unaogharimu jumla ya dola milionni 7.1 utatoa huduma kwenye wilaya kadha kwenye mikoa ya Gauteng na KwaZulu-Natal ambapo utatoa huduma za kuzui maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na huduma zingine kwa wafanyikazi wahamiaji na kwa wenyeji. Kati ya athari za kiafya zinazowakabili wafanyikazi wahamiaji ni pamoja na misongamano na hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kifua kikuu.

Zaidi ya wahamiaji 20,000 wamepata huduma za kiafya kipitia mradi huo tangu ulipoanzishwa mwaka 2009.

(CLIP: Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM)