Siku ya wajane duniani kusherehekewa kesho

22 Juni 2012

Siku ya kimataifa ya wajane ilibuniwa mwaka 2005 kupitia usaidizi wa wakfu wa Loomba na kutambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2010. Wakfu wa Loomba ulibuniwa mwaka 1997 na Lord Raj Loomba kama njia ya kumkumba mamake ambaye alibaki mjane akiwa na umri wa miaka 37 eneo la Punjab nchini India.

Wakfu huo unalenga kuwaelimisha watoto wa waajane maskini na kuwainua wajane kote duniani. Tangu kubuniwa kwa siku ya wajane duniani mwaka 2005 wakfu huo umewaelimisha maelfu ya watoto wa wajane maskini na kuwasaidia zaidi ya watu 27,000 wa familia zao.

Siku hii itasherehekewa mjini New York tarehe 23 mwezi huu ambapo farasi watabeba watu kwenye eneo la Central Park kwenye shughuli inayofadhiliwa na wakfu wa Loomba.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter