Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ataka haki za waathiriwa wa ugaidi kushughulikiwa

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ataka haki za waathiriwa wa ugaidi kushughulikiwa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamku na vita dhidi ya ugaidi Ben Emmerson ameshauri serikali kote duniani ambazo zinakabiliwa na hatari ya ugaidi kulinda kwa pamoja haki za waathiriwa wa ugaidi. Emmerson amesema kuwa ugaidi una athari za moja kwa moja kwa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi.

Akiongea alipokuwa akiwasilisha ripoti yake ya kila mwaka kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Emmerson amesema hata baada ya kuwepo njia za kupamana na ugaidi duniani bado haijapatikana njia ya kushughulikia haki za waathiriwa wa ugaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)