Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya usalama ni kikwazo kwa operesheni za UM Syria:

Matatizo ya usalama ni kikwazo kwa operesheni za UM Syria:

Hatua ya kupelekwa wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Syria imesitishwa kwa muda kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kurtibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanatafuta njia mbadala ya kufikisha msaada ikiwemo kuashisha ushirikiano na mashirika ya misaada ya nchini humo. Mapema mwezi huu serikali ya Syria ilikubali kupeleka wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa katika majimbo manne yaliyoathirika zaidi na vita.

Kwa mujibu wa msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema mapigano yaliyoongezeka siku za karibuni yanazuia uwezo wa mashirika ya Umoja wa myaifa ya misaada kufanya kazi yake na kupeleka wafanyakazi wake kunakotakiwa.Amesema misaada ya kitaifa imepungua na kuna fursa ndogo ya kuyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi na mapigano.

(SAUTI YA JENS LAERKE)