Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa nchini Lebanon

Ban akaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa nchini Lebanon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa kati ya viongozi wa kisiasa nchini Lebanon. Kupitia kwa msemaji wake Ban amewashauri viongozi wa kisiasa nchini Lebanon kuendelea na kazi yao kwenye mpango huu muhimu wanapojiandaa kwa mkutano unaopangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu.

Kulingana na vyombo vya habari mkutano ulioandaliwa chini ya uenyekiti wa rais wa Lebanon Michel Sleiman mnamo Juni 11 kati ya viongozi wa kundi la Hizbollah ni wa kwanza wa kitaifa kundaliwa kwa muda wa miezi 18 iliyopita ambapo viongozi walikubaliana kujitolea na kujizuia na hotuba ambazo zinaweza kuleta chuki.