Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu ataka nchi maskini zisaidiwe kufikia shabaha ya maendeleo endelevu

Rais wa Baraza Kuu ataka nchi maskini zisaidiwe kufikia shabaha ya maendeleo endelevu

 

Mashirikiano ya kimaendeleo lazima yaweka kipaumbele kuzisaidia nchi maskini kutekeleza sera zinazoangazia maendeleo endelevu.

Huo ndiyo ujumbe mahususi uliotolewa na rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Nasir Abdulaziz Al-Nasser wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa Rio + 20, unaofanyika huko Brazil.

Amesema kuwa bado nchi masikini zinapaswa kuungwa mkono kwa kupatiwa misaada zaidi kwani bila kufanya hivyo kunaweza kukabiliwa na hali ya mkwamo kwenye ufikiaji wa dhana ya maendeleo endelevu. Amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na dhamira ya dhati ili kutekeleza kwa vitendo malengo yote yaliyoanishwa na mkutano wa Rio + 20.