Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malawi inahitaji kusikia haki zao zitaheshimiwa:Kang

Malawi inahitaji kusikia haki zao zitaheshimiwa:Kang

Malawi imepitia changamoto kubwa na ngumu katika miaka ya karibuni lakini mabadiliko ya amani ya serikali ni moja ya dalili njema zinazoashirika maisha bora ya baadaye.

Kauli hiyo imetolewa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang wakati akikamilisha ziara yake nchini humo.

Bi Kang amesema wakati taifa hilo linainuka kutoka katika matatizo na mabadiliko ya kisiasa Wamalawi wanahitaji kusikia kutoka kwa viongozi wao kwamba haki zao za msingi za uhru wa kujieleza, kukusanyika na kujmuika zitaheshimiwa na wanataka kuona hatua madhbuti zinachukuliwa kudhihirisha haya.