Kenya itatimiza muafaka wa Rio+20:Kibaki

21 Juni 2012

 

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema jumuiya ya kimataifa imekutana tena Rio Brazili ili kutoka na muafaka wa kisiasa kwa ajili ya maendeleo endelevu na kutokomeza umasikini.

Na amweuhakikishia ulimwengu kupitia hoptuba yake kwamba taifa la Kenya litakuwa kinara katika kuhakikisha dunia inakuwa na mstakhbali mzri wenye manufaa kwa wote.

Amesema ingawa hatua zimepigwa za kichumi duniani lakini hazilingani hasa katika kufikia malengo na pia kutimiza ahadi walizokubaliana viongozi wa dunia.

Hivyo amesema sera bora za kujali mazingira zitatoa fursa za kongeza uzalishaji, ajira bora, kupnguza umasikini, kulinda mazingira na kuleta maendeleo ya kichumi kwa faida ya wote.

(SAUTI YA MWAI KIBAKI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter