Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushambulia waandishi ni kushambulia demokrasia

Kushambulia waandishi ni kushambulia demokrasia

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa wamelaani idadi kubwa ya maaji ya waandishi wa habari au hali ya kutowatendea utu kutokana na uwajibikaji wao.

Frank La Rue mtaalamu wa uhuru wa maoni na kujieleza na Christof Heyns mtalamu kuhusu mauaji ya kunyongwa au y kiholea wamezitaka serikali kote dniani kuchukua hatua kuwalinda waandishi wa habari na uhru wa vyombo vya habari.

Katika ripoti yao kwenye baraza la haki za binadamu wataalamu hao wawili wamesema waandishi wa habari wanazidi kukabiliwa na ukikaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kupokea vitisho vya kuuawa, kukamatwa, kuteswa, kuawa, na ukatili wa kimapenzi dhidi ya waandishi wanawake.

 Bwana La Rue ametoa wito wa kukomeshwa utumizji wa sheria za kuchafuliana majina, usalama wa taifa na za kupinga ugaidi kwa kwakandamiza na kuwakosoa waandishi,kwani amesema zinaweza mazingira ya woga na kuchagiza udhibiti binafsi kwa wandishi.

(SAUTI YA FRANK LA RUE)