Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aweka malengo matatu kutimizwa ifikapo 2030

Ban aweka malengo matatu kutimizwa ifikapo 2030

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema viongozi wa duunia wamekusanyika Rio ili kuunda mfumo mpya wa kimataifa. Ban ameyasema hayo Alhamisi wakati wa utiaji saini makubaliano ya kuanzishwa taasisi ya kimataiga ya kuaji unaojali mazingira.

Amesema ameweka malengo makubwa matatu kwa ajili ya kutimizwa ifikapo 2030. Malengo hayo ni moja fursa ya nishati kwa wote, pili kuongeza mara mbili kiwango cha upatikanaji nishati dniani na tatu kuongeza mara mbili uwezo wa kuwa na nishati mbadala duniani.

Ban amesema kwa kwapa watu nishati safi dunia itakuwa inachagiza maendeleo ,kupambana na hali ya kutokuwepo kwa usawa, na klinda mazingira. Na ameongeza kuwa nishati endelevu kwa wote itawapa watu zaidi ya bilioni moja fursa ya kuwa na nishati ya kisasa.

Nishati ni moja ya mada nyingi zinazojadiliwa kwenye mkutano wa Rio+20, mengine ni usawa wa kijinsia, ukuaji wa miji, elimu, ukosefu wa chakla na matatizo mengine yanayohitaji hatua za haraka.