Benki kubwa zaidi zaahidi bilioni kwa uchukuzi endelevu, kwenye Rio+20

20 Juni 2012

Benki 8 kubwa zaidi za maendeleo duniani zimejitolea kuwekeza dola bilioni 175 katika kusaidia kuweka miundo ya uchukuzi endelevu kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Benki hizo ni Benki ya Asia, Benki ya Dunia na benki zingine sita za maendeleo. Kujitolea kwa benki hizi katika kufanya hili, kutasaidia kuchangia hewa safi and barabara salama.

Tangazo hilo limefanywa Jumatano kwenye mkutano wa kimataifa wa maendeleo endelevu wa Rio+20.

Harujiko Kuroda ni rais wa Benki ya Maendeleo ya Asia.

“Katika nchi zinazoendelea, kuna kati ya magari 10-30 kwa kila watu 1, 000 sasa, ukilinganisha na 600 hadi 800 kwa mataifa mengi yaliyostawi. Kadri vipato vya watu vinavyopanda, ndivyo ongezeko la magari litakuwepo haraka sana.

Lakini nchi hizi zinazoendelea zinaweza kuruka mara moja na kuingia maendeleo safi kwa mazingira, yenye vyombo vichache zaidi vya injini, safari fupi na salama zaidi, na mifumo ya usafiri inayohifadhi nishati, na hivyo kuendeleza afya na hali ya maisha ya watu wazo.”