Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanzilisha wa chama cha kijani Brazil ataka UNEP kupewa zingatio zaidi

Mwanzilisha wa chama cha kijani Brazil ataka UNEP kupewa zingatio zaidi

Mwanzilishi wa chama kimoja cha kimazingira nchini Brazil Fernando Gabeira amesema kuwa kongamano la Rio +20 inapaswa kujadilia kwa kina nafasi ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nafasi yake ya kukabiliana changamoto za dunia juu ya mazingira na uoto wake.

Fernando ambaye anashika nafasi ya mbele kabisa kuhusiana na utetezi wa mazingira amesisitiza kuwa UNEP inapaswa kupewa kipaumbele kushughulikia changamoto za kimazingira inayoendelea kuindama dunia.

Katika mahojiano yake mafupi na Redio Umoja wa Mataifa, amesema kuwa anamatazamio makubwa kuhusiano na mkutano huo.

Ametaka kufanyika mabadiliko makubwa juu ya chombo hicho cha kimataifa ili hatimaye kuzalishe tija zinazotarajiwa.