Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kuchunguza ongezeko la acid baharini

IAEA kuchunguza ongezeko la acid baharini

Ongezeko la gesi ya Cabon dioxide hewani kumesababisha bahari duniani kuwa na acid nyingi ambayo inatishia mfumo wa maisha ya vimbe wa majini.

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linasaidia utafiti na kuchukua hatua kuhsu tatizo hilo kwa kuanzisha kituo cha kimataifa cha uratibu wa masuala ya acid baharini na maabara yake aambachi kitakuwa Monaco.

Kituo hicho kimezinduliwa rasmi kwenye mkutano wa Rio+20 ulioanza rasmi Jumatano mjini Rio de Janairo Brazil.