Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa maziwa makuu Tanzania warudi nyumbani

Wakimbizi wa maziwa makuu Tanzania warudi nyumbani

Wakati dunia hii leo inaadhimisha siku ya wakimbizi ambako kunasisitizwa kuepusha madhira yanayoweza kuzalisha watu wa jamii hiyo, idadi kubwa ya wakimbizi kutoka eneo la maziwa makuu sasa wameanza kurejea nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa kipindi kirefu

Huko nchini Tanzania ambako kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikihifadhi wakimbizi kutoka nchi za Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Somalia ripoti zinaonyesha kuanza kupungua kwa idadi ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao.

Wakimbizi walioko sasa wamehifadhiwa katika kambi za Nyarugusu na Mtabila zilizoko Mkoani Kigoma, na wengine wamepatiwa hifadhi katika eneo la Chongo lililoko Mkoani Tanga ambalo linachukua idadi ndogo ya wakimbizi kutoka nchini Somalia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatiwa moyo na mwenendo wa kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao hasa katika nchi zile ambazo zimefaulu kuvuka kipindi kigumu cha migogoro ya kivita na ukosefu wa utashi wa kisiasa. Kulingana na Bwana Austine Makani ambaye ni afisa habari wa UNHCR, kuna matumaini makunbwa ya kuendelea kupungua idadi ya wakimbizi hao nchini Tanzania.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAKANI)