Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri viumbe wa majini:UNDP

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri viumbe wa majini:UNDP

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP limechapisha taarifa mpya khusu hatari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa kwa vimbe wa majini.

Taatrifa hiyo iitwayo uangalizi wa mabadiliko ya hali ya hewa na maisha ya vimbe wa majini imebaini kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia maisha ya mabilioni ya watu duniani ambao wanategemea dola trilioni 12 zinazotokana na viumbe wa majini kila mwaka.

UNDP inasema ongezeko la hatari na athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika bahari zinahitaji dunia kuwekeza haraka katika chumi unaojali mazingira ambapo nchi zitafikia malengo ya maendeleo katik njia muafaka, huku wakati huohuo zikitimiza mahitaji ya watu wake.