Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya chakula ni zaidi ya kujilinda na njaa:De Schutter

Haki ya chakula ni zaidi ya kujilinda na njaa:De Schutter

Mtaalam Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na chakula, Olivier De Schutter, ameunga mkono muafaka ulofikiwa kuhusu mkataba wa Rio+20. Amesema, wahusika wametambua mchango muhimu wa haki za binadamu, ikiwemo haki ya kuwa na chakula, katika kuwa na maendeleo endelevu.

Ameelezea kuzingatiwa kwa haki ya kuwa na chakula katika mswanda huo kama jambo muhimu sana. George njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)