Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yawasilisha mpango kuhusu ujenzi wa soko la siku za usoni

UNDP yawasilisha mpango kuhusu ujenzi wa soko la siku za usoni

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limewasilisha mpango mkakati wenye shabaha ya kuinua hali ya kilimo katika nchi zinazoinukia kiuchumi kwa kusisitiza haja ya kuwepo mashirikiano baina ya serikali, wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo.

Mpango huo ambao unatupia macho zaidi kilimo endelelevu unapendelea kuona kuwa sehemu hizo zinajenga daraja la pamoja na hatimaye kuratibu uzalishaji wa mazao ili kuongeza kasi ya soko la nje kwa mazao kama kahawa, kokoa na mazao mengine ya nafaka.

Katika mpango huo UNDP imetumia maneno yasomekayo ujenzi wa soko la siku za usoni kama sehemu ya kuupa msukumo zaidi mpango huo ambao umefadhiliwa na mataifa kadhaa ikiwemo Denmark, Ghana, Indonesia.

Lengo kubwa la hatua hiyo ni kuzisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki yatayowezesha sekta za umma na zile binafasi zinashirikiana kwa karibu na kuinua kiwango cha uzalishaji wa mazao