Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasafirisha misaada kwa wakimbzi wa Sudan walio jimbo la Upper Nile

UNHCR yasafirisha misaada kwa wakimbzi wa Sudan walio jimbo la Upper Nile

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanzisha shughuli mpya ya dharura ya kusafirisha misaada kwa njia ya ndege kwenda kwa wakimbizi walio kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini.

Shughuli hiyo inalenga kuwapelekea misaada wakimbizi 50,000 ambao wamekimbia mizozo na uhaba wa chakula kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan.

Ndege ya shirika la UNHCR imekuwa ikifanya safari mara mbili kwa siku ikisafirisha misaada kutoka mjini Juba kwenda uwanja mdogo wa Paloich ulio umbali wa kilomita 90 kutoka kambi ya wakimbizi ya Jammam. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(CLIP YA ADRIAN EDWARDS)