Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa dunia lazima wasikilizwe Rio+20

Wanawake wa dunia lazima wasikilizwe Rio+20

Kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN women kupitia mkurugenzi wake mkuu Michele Bachelet kimesisitiza kwamba sauti za wanawake lazima zisikilizwe.

Akizungmza kwenye mkutano wa Rio+20 Bi Bachelet amesema dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimazingiza na ili kukabiliana nazo ni lazima wanawake washirikishwe na sati zao zipewe nafasi.

Makundi mbalimbali yanayojumuisha wanawake yako Rio De Janeiro kwenye mkutano ili kfikishwa matakwa yao.

Patricia Kuya ni miongoni mwa wanawake wanaohudhuri mkutano huo akiwakilisha kundi la kina mama wa Afrika na anatokea nchini Tanzania.

(MAHOJIANO NA PATRICIA KUYA)