Baraza la Usalama lalani vikali mashambulizi ya askari waasi DRC

18 Juni 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali matukio ya mashambulizi yaliyofanywa na kundi la askari walioasihuko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kusababisha mauwaji ya watu kadhaa.

Askari hao wameripotiwa kufanya mashambulizina kuwauwa raia kadhaa wakiwemo wanawake na watoto na kushiriki vitendovya kuwanyanyasa wananchi.

Katika eneo hilo la kusini na kaskazinimwa jimbo la Kivu, askari hao waasi wanaendelea kushambuliana na vikosivya serikali ambavyo vimeweka shabaha ya kumkamata kiongozi wa askari hao Bosco Ntaganda.

Kiasi cha watu 100,000 wanaripotiwa kukosamakazi kutokana na ghasia hizo na baadhi yao wamekimbilia maeneo ya mbali.

Katika taarifa yake, baraza hilo la usalama pamoja na kulaani mauwaji hayo ya wananchi lakini pia limetaka uungwajimkono toka kwa nchi jirani ili kukabiliana na waasi hao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter