Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waangalizi wa UM nchini Syria wasitisha shughuli

Waangalizi wa UM nchini Syria wasitisha shughuli

Waangalizi wa kimataifa kwa ajili ya mzozo wa Syria wamesitisha shughuli zake nchini humo kutokanana idadi ya mashambulizi ya silaha kuwa ya kiwango cha juu.

Taarifa iliyomkariri Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Generali Robert Mood imesemakuwa kuwamekuwa na ongezeko la mashambulizi karibu katika eneo nzima laSyria na hivyo kuzuai kwa kiwango kikubwa shughuli za uangalizi wa haliya mambo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamezilaumu pande zinazohasimiana kwa kushindwa kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya kurejea mezani kwa majadiliano na badala yake pandehizo zimeendelea kujibizana kwa silaha.

Kutokana na kuzidikushamiri kwa mashambulizi waangalizi hao wa Umoja wa Mataifa sasa wataendeleakusalia katika sehemu maalumu huku wakisitisha misafara yote ikiwemo ileya upigaji doria.