Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN Women azungumzia mustakhbali wa wanawake kwenye Rio+20

Mkuu wa UN Women azungumzia mustakhbali wa wanawake kwenye Rio+20

 

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women Bi Michele Bachelet, akizungumza na waandishi wa habari mjini Rio De Jenairo Brazili, ameelezea mustakhbali wanaotaka wanawake.

Katika mkutano huo wa Rio+20, amesema wakati wanawake wakifurahia haki sawa, fursa sawa na ushirikishwaji, wanaweza kuchangia pakubwa katika maendeleo endelevu.

Ameongeza kuwa ushirikishwaji kikamilifu na sawia wa wanawake unazifanya jamii, uchumi na mazingira kuwa bora zaidi.

Bi Bachelet amesema dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, tofauti za kijamii na uharibifu wa mazingira, na wanawake wako Rio kuhakikisha sauti zao zinasikilizwa na kuubainishia ulimwengu ni mustakhbali wa aina gani wanaotaka.

(SAUTI YA MICHELE BACHELET)