Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNSMIS ataka pande hasimu kuruhusu raia kuondoka maeneo ya vita Syria

Mkuu wa UNSMIS ataka pande hasimu kuruhusu raia kuondoka maeneo ya vita Syria

Wakati huo huo raia wanaendelea kukwama kutokana na machafuko yaliyoshika kasi Syria amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi Syria UNSMIS Jenerali Robert Mood.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumapili jioni Mood amesema katika mji wa Homs juhudi za kuwaondoa raia wanaozingirwa na mapigano zimeshindwa kuzaa matunda.

Amezitaka pande zote husika katika vita kufikiria upya na kuwaruhusu wanawake, watoto, wazee na majeruhi kuondoka katika maeneo ya mapigano, bila masharti yoyote na kuhakikisha usalama wao. Amesema hatua hiyo inahitaji tashi ktoka pande zote wa kuheshimu na klinda maisha ya watu wa Syria.

(SAUTI YA JENERALI MOOD)