Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yapendekeza ruzuku wastani kwa wote

ILO yapendekeza ruzuku wastani kwa wote

Shirika la Wafanyakazi Duniani, ILO, limependekeza kuwekwe ruzuku wastani ya kijamii kwa watu wote, ili kuwasaidia zaidi ya watu bilioni 5 wasiojiweza kukidhi mahitaji muhimu kama ya afya na mengineyo.

Hii ni kwa kufuatia maazimio mapya yaliyokubaliwa mwishoni mwa kongamano la kimataifa la wafanyakazi.

Shirika la ILO limesema kuwekwa kwa kiwango cha wastani cha ruzuku ya kijamii, kitawasaidia watu kukidhi mahitaji ya afya katika maisha yao yote, na kuchangia kupunguza umaskini, tofauti za riziki, na watu kufa mapema.

 Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Juan Somavia ruzuku ya kijamii itawapa watu uwezo na kuchangia ukuaji wa uchumi.