Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia Syria zinazuia kazi za UNSMIS:Mood

Ghasia Syria zinazuia kazi za UNSMIS:Mood

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Jenerali Robert Mood, amesema kuwa kuongezeka kwa ghasia kunazuia kazi ya waangalizi hao.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ndiyo sehemu pekee ya mpango wa amani wa kimataifa wenye lengo la kurejesha utulivu katika taifa hilo ambako mzozo unaendelea kuwa mbaya zaidi.

Jenerali Mood amezilaumu pande zote za mzozo huo kwa kuchangia kuoengezeka umwagikaji damu. Amesema wahusika wote wameongeza ghasia maksudi, na kuchangia hasara na vifo kwa pande zote, na kuwaweka waangalizi hatarini.

(SAUTI YA GENERAL MOOD)