Washauri wa Ban wahofia mauaji yanayoendelea Syria

15 Juni 2012

Washauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon wanaohusika na kuzuia mauaji ya halaiki na jukumu la kulinda mabwana Francis Deng na Edward Luck wameelezea wasi wasi uliopo kutokana na ripoti za kuuawa kwa watu wengi kwenye uvamizi nchini Syria.

Kwenye taarifa yao washauri hao wamesema kuwa uvamizi huo ulihusisha mashambulizi yaliyoendeshwa na serikali na makundi mengine kwenye maeneo ya raia na kwenuye mali ya raia ambayo yanaweza kutajwa kuwa uhalifu dhidi ya kibinadamu.

Wanasema kuwa mauaji haya ni ishara ya kushindwa kwa serikali ya Syria katika kuwalinda raia wake.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter