Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo viondolewe Gaza:UM na wadau wengine

Vikwazo viondolewe Gaza:UM na wadau wengine

Mashirika hamsini ya kimaifa ya kutoa misaada pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa kauli moja ya kuondelewa kwa vikwazo Gaza.

Mashirika hayo yamechapisha taarifa fupi katika kuadhimisha kukumbukumu ya miaka mitano ya kuongeza nguvu vikwazo hivi. Taarifa hiyo inasema; Kwa zaidi ya miaka mitano Gaza, zaidi ya watu milioni 1.6 wameishi chini ya vikwazo na ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa, Zaidi ya nusu ya watu hawa ni watoto.

Sisi ambao tunasaini taarifa hii tunasema kwa kauli moja "sitisha vikwazo sasa hivi". Serikali ya Israel inakabiliwa na upinzani wa kimataifa dhidi ya vikwazo Gaza na taarifa hii ya kauli moja kutoka kwa  baadhi ya mashirika ya kimataifa yanayoheshimiwa sana duniani ina uwezo wa kuongeza shinikizo ili vikwazo viondolewe.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada na ya maendeleo ambayo yametia saini taarifa hii ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kiraia.